Kenya Literature Bureau

 (+254) 20 3541196/7

Hot Books

Let Her Be

 

 

Nasaha Kamusi Ya Vitendawili Na Mafumbo ni kitabu ambacho kimekusanya vitendawili na mafumbo yaliyopangwa kimaudhui. Vitendawili na mafumbo ni sehemu muhimu katika maisha na maendeleo ya mwanadamu hususan katika kukuza lugha na kuhifadhi utamaduni.

Vitendawili na Mafumbo humtangamanisha mwanadamu na mazingira yake kikamilifu akaishia kuyasoma, kuyatafiti na kuyaonea fahari.

Utegaji na uteguaji wa vitendawili pamoja na ufumbaji na ufumbuaji wa mafumbo humfikirisha mtu na kutathmini uzoefu wake wa maisha kijumla. Aliyezoea vitendawili na mafumbo; kwa kusema au kusoma, huishia kuogelea bahari hiyo pasina ugumu wowote.

Lugha ya Kiswahili inapokosa vitendawili na mafumbo inakuwa ni kama barabara iliyojengwa ila haitumiwi.